Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taboa wapata safu mpya ya viongozi

22316 Taboa+pic TanzaniaWeb

Mon, 15 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) wamefanya uchaguzi wa kupata safu mpya ya uongozi kwa miaka mitatu ijayo baada ya uliopita kumaliza muda wake.

Katibu wa kamati ya uchaguzi, Omary Chaka  amesema katika uchaguzi huo uliofanyika leo, wajumbe wamemchagua Mohammed Abdallah kuwa mwenyekiti mpya wa Taboa akichukua nafasi ya Mohammed Hood aliyemaliza muda wake baada ya kudumu kwa miaka saba.

Abdallah  ambaye alikuwa makamu wa mwenyekiti wa uongozi uliopita alipata kura 46 kati ya 52 zilizopigwa, huku mshindani wake Miraji Ally akiambulia kura nne.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu ametetea nafasi yake baada ya kupata kura 48 kati ya 52 zilizopigwa akiwa ni mgombea pekee.

Katibu wa uchaguzi huo, Chaka alisema nafasi ya katibu mkuu msaidizi imechukuliwa na Joseph John aliyepata kura 44 kati ya 55 akiwa mgombea pekee.

Chaka alisema nafasi ya mweka hazina imechukuliwa na Issa Nkya kwa kupata kura 48 ambaye ametetea nafasi hiyo, huku msaidizi wake akiwa ni Mbazi Mjema akipata kura 49 kati ya 52.

Akizungumza na waandishi wa habari, Abdallah alisema atahakikisha anafanya kazi karibu na Serikali katika utekelezaji  wa majukumu yake.

"Sitowaangusha kwenye uongozi na mmepata mtu sahihi na Serikali itajua kuwa kuna kiongozi mfuatiliaji wa Taboa," alisema Abdallah.

Kwa upande wake, Mrutu aliwahidi wajumbe hao kutorudi nyuma katika utelezaji wa majukumu yake hasa suala la mabasi kulala njiani.

Chanzo: mwananchi.co.tz