Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi za Serikali Mbeya zadaiwa mabilioni ya ankara za maji

81349 Pic+madeni Taasisi za Serikali Mbeya zadaiwa mabilioni ya ankara za maji

Wed, 23 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya (Mbeya-Uwas) imesema inashindwa kutekeleza baadhi ya miradi ya maji kutokana na kuzidai taasisi za Serikali Sh1.5 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 23, 2019 na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo, Ndele Mengo.

Amesema kuwa licha ya kufuatilia madeni hayo katika taasisi hizo za Polisi, Magereza, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vituo vya afya ulipaji hauridhishi.

“Kama polisi tunadai zaidi ya Sh657 milioni, JWTZ 43.9 milioni, Magereza Mkoa Sh631.9 milioni, Chuo cha Magereza 225.8 milioni.

Amesema kutokana na deni hilo baadhi ya miradi imekuwa changamoto kwa kuwa mamlaka hiyo inategemea mapato yake ya ndani kujiendesha na kulipa mishahara.

Chanzo: mwananchi.co.tz