Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi ya Kapuya yapigwa Marufuku kwa ukiukaji wa Sheria

Athuman Kapuya Foundation Taasisi ya Kapuya yapigwa Marufuku kwa ukiukaji wa Sheria

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Msajili kupitia Bodi ya uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yaani (Non Government Organization) imesisamisha utendaji kazi wa shirika la Athuman Kapuya Foundation kutokana uendeshaji wake kwenda kinyume na mila na Desturi za Tanzania.

Kupitia Taarifa iliyotolewa leo Juni 04,2024 na Ofisi ya Msajili kupitia Bodi ya uratibu wa mashirikia yasiyo ya kiserikali yaani (Non- Government Organization) imesema.

Shirika hilo limekua likifanyakazi kinyume na katiba waliyosajili na kinyume cha sheria ya Usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ( NGO's).

Aidha Taarifa hiyo imempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Paul Chacha kwa uratibu mzuri wa Mashirika yanayofanya kazi katika mkoa wa Tabora na hatua alizochukua kama Mamlaka kamili ya Usimamizi wa Shughuli za Serikali mitaa baada ya kuibua madhaifu ya Shirika la Athuman Kapuya Foundation.

Ofisi hiyo imetoa wito kwa Mamlaka zote za tawala mikoa na Mamlaka za Serikali kuimarisha uratibu na kuchukua hatua stahiki pale wanapoona kuna ukiukwaji wa Sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live