Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Taarifa ya msichana kuvuliwa nguo ni potofu" -RPC

RPC MARA Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP Longinus Tibishubwamu

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Mara limesema kwamba Askari wake wamekuwa wakitenda majukumu yao kwa weledi na kwamba tukio la msichana kutendewa isivyo kwa kuvuliwa nguo ni la kutengenezwa halina ukweli wowote.

Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP Longinus Tibishubwamu, kupitia mkutano ulioandaliwa kwa njia ya mtandao.

"Askari wetu wanafanya kazi kwa weledi na watu wanaotupiga vita hilo tukio (tuhuma za binti kutotendewa isivyo stahili) wamelipika hicho kitu hakipo, hilo limepikwa ili kuchafua kazi nzuri ya jeshi la polisi, hivyo taarifa ya msichana sijui kuvuliwa nguo ni potofu na kwa ujumla mkoa wa Mara ni shwari," amesema Kamanda Tibishubwamu

"Taarifa za upotoshaji kuhusu utendaji wetu wa kazi naomba wananchi wazipuuze na wale wanaotoa taarifa zile wapuuzwe kwa sababu ni ajabu mtu mwenye akili timamu kutetea jambazi linaloua na kupora watu kwa bunduki ya kivita," ameongeza Kamanda Tibishubwamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live