Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TaCRI kumkumbuka Magufuli kwa kuwezesha utafiti

532c73ca804b280dee835c3246e62b0a TaCRI kumkumbuka Magufuli kwa kuwezesha utafiti

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Utafiti wa Zao la Kahawa nchini (TaCRI), imesema itamkumbuka Rais John Magufuli kwa mchango wake wa kuwekeza katika tafiti mbalimbali za zao hilo, hatua ambayo imesaidia kugundulika kwa aina nyingi bora za kahawa zenye uhakika katika soko la dunia.

Taasisi hiyo imegundua aina bora za mbegu za kahawa zenye uwezo wa kukinzana na mgonjwa mbalimbali na zenye kuhimili ukame zipatazo 23 ambapo aina ya Arabika 19 na Robusta nne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi zake zenye makao makuu Lyamungo, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TaCRI, Dk Deusdedit Kilambo, alisema taasisi hiyo itamkumbuka Magufuli katika harakati zake za kuinua zao la kahawa.

“Kifo cha Magufuli ni pigo kwa taifa maana tunaelewa namna alivyokuwa na misimamo...lakini sisi kama TaCRI ambao ni watafiti wa kahawa na wasambazaji wa matokeo ya utafiti tutamkumbuka katika jitihada zake alizotusaidia na alitimiza jukumu hili kwa njia pana zaidi,” alisema.

Alisema Kahawa inalimwa katika mikoa 16 nchini na kwamba katika maeneo yote Magufuli alihimiza wakulima kutumia matokeo ya utafiti ambayo yanaongeza tija na ubora wa kahawa.

“Serikali imekuwa mdau mkubwa kwa taasisi hii ambapo imekuwa ikitoa fedha na tunaamini ilikuwa ni kupitia maagizo yake... fedha zimekuwa zikitusaidia kuendesha shughuli za utafiti na kueneza matokeo ya tafiti ambazo zimesaidia wakulima kupata tija,” alisema.

Hata hivyo, Dk Kilambo alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na kumuomba kutupia jicho katika taasisi mbalimbali za utafiti haswa za kilimo jambo ambalo litasaidia nchi kupiga hatua katika sekta ya Kokomo.

Mbali na hilo alisema jukumu kubwa la taasisi hiyo ni kutoa aina bora za kahawa zinazokidhi mahitaji ya soko ambapo kwa sasa wamefanikiwa kugundua Aina 23 bora ambapo katika nchi Afrka Mashariki wanashikilia nafasi ya Kwanza.

“Kwa Afrika Mashariki tunashikilia nafasi ya kwanza na duniani nchi zinazofanya utafiti wa kahawa ni 60 na katika hizo sisi tunashikilia nafasi ya nane...jambo hili ni zuri na tuna imani Rais Samia ataendelea kutusaidia zaidi,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz