Shirika la UNESCO kwa ufadhiri wa Koica kupita mradi wa kuwaweze wasichana walio katika umri wa balehe na akina mama wadogo kupitia elimu nchini Tanzania wamejenga kituo cha malezi na makuzi ya watoto chenye thamani ya Sh73.3 milioni kilichojengwa kata ya mwabaluhi Wilayani Sengerema.
Mkurugenzi mkazi na mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Tirso dos Santos amesema mradi huu umelenga kuboresha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto wilayani Sengerema kupitia kata tano.
Amezitaja kata hizo kuwa ni Mwabaluhi, Nyatukala, Ibisageni, Mission na Nyampulukano ambazo zilichaguliwa kama kata za majaribio.
Tirso dos Santos amesema mradi huu kwa Tanzania Bara unatekelezwa kwenye Wilaya tatu za mfano ambazo ni Sengerema, KasuLu na Ngorongoro.
"Ninawaomba wananchi kuutunza mradi huu na kuwaleta watoto kuanzi miaka 2 hadi 4 lengo nikutapata malezi bora" amesema Tirso dos Santos.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Aberi Mosho amesema kituo hiki kimejengwa kwa miezi kumi pekee na wananchi wamechangia nguvu kazi.
Amesema huduma zitakazo tolewa kwenye mradi huu ni malezi ya watoto na makuzi ya watoto pekee hivyo awaomba wananchi Wilayani Sengerema kuwaleta watoto wao Ili wapete malezi mema.
Ofisa ustawi wa jamii Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, Nyanjige Julius amesema kituo hiki cha kulea watoto kitahudumia watoto 50 kwampigo hivyo anaiomba jamii kujitokeza kuleta watoto kwenye kituo hiki.
Mmoja wa wakazi Wilayani Sengerema Sarah John amesema mradi huu utakuwa mkombozi kwa Wananchi hivyo tunatakiwa kuutunza na kuuthamani.
Gabriela Lukas mratibu wa mradi wa kuwawezesha wasichana walio katika umri balehe na akimama wadogo amesema mradi huu utakuwa chachu ya maendeleo kwa wanasengerema na Wananchi hivyo Wananchi wanataliwa kupeleka watoto kwenye kituo hicho.