Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC Dodoma yasitisha safari, uuzaji wa tiketi za treni

90613 Treni+pic TRC Dodoma yasitisha safari, uuzaji wa tiketi za treni

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mkoa wa Dodoma limesitisha uuzaji wa tiketi kwa wasafiri wa treni hadi itakapotoa taarifa.

Chanzo cha kusitisha uuzaji wa tiketi ni kutokana na eneo la Godegode – Gulwe mkoani humo kutoruhusu treni kupita na mafundi bado wanashughulikia.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 2, 2020, stesheni Masta wa kituo cha Dodoma Rose Ngauga amesema ili kuepuka gharama ambazo zinaweza kuzuilika wamechukua uamuzi wa kusitisha uuzaji wa tiketi kwa muda.

Ngauga amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya eneo la Godegode –Gulwe Wilaya ya Mpwapwa kwenda Dar es Salaam kuendelea kujaa maji pamoja na mchanga.

Kwa miaka mingi eneo la Godegode limekuwa ni korofi katika msimu wa mvua na kusababisha mara nyingi treni kusitisha safari zake kutokana na maji yanayoshuka kutoka milima ya Kibakwe kuharibu miundombinu.

“Tumeamua kusitisha uuzaji wa tiketi kwa muda, hii itasaidia pia kutowaweka wananchi muda mrefu, pamoja na gharama nyingine ambazo zinaweza kujitokeza,” alisema Ngauga.

Ngauga amesema kuna treni inatarajiwa kuanza safari kesho Ijumaa Januari 3, 2020 saa tisa alasiri wakiamini matengenezo katika njia ya reli yatakamilika.

Aidha amesema hadi kesho asubuhi Januari 3, 2019 atapata majibu kamili matengenezo hayo yamekamilika au laa na kama yatakuwa yamekamilika ataanza kuuza tiketi.

Jumatatu iliyopita ya Desemba 30, 2019 jioni abiria waliokuwa wakitokea mkoani Kigoma kwenda Dar es salaam walikwama mkoani Dodoma kutokana na mvua zinazoendelea kusababisha madhara ya kujaa maji na mchanga katika maeneo mbalimbali ya reli, ambapo juzi Jumanne Desemba 31, 2019 walitafutiwa usafiri wa magari ili kuendelea na safari.

Chanzo: mwananchi.co.tz