Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPDC yawashika mkono wanakijiji Mtendachi

Tpc Pic TPDC yawashika mkono wanakijiji Mtendachi

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: mwanachidigital

hirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetoa Sh20 milioni ili kuchangia ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mtendachi ambayo inajengwa kwa nguvu za wananchi ili kusogeza huduma za afya kijijini hapo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Ofisa Maendeleo ya Jamii wa TPDC Eugine Isaya amesema kuwa shirika hilo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inayozunguka miradi ya gesi inapata huduma na kwamba kiji hicho kipo jirani na kiwanda cha kuchakata gesi Madimba.

“Tulipata maombi yao na tumetoa baada ya kuona wananchi wanania ya kupata huduma ya zahanati, nah ii siyo mara kwanza kwani hata kijiji cha Mngoji tumejenga zahanati japo bado haijafunguliwa. Sisi huwa tunachangia kwa miradi iliyoibuliwa na wanchi wenyewe,” amesema Issaya.

kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanaf Msabaha, amewataka wananchi kujitoa Zaidi na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo na hivyo kuanza kupata huduma kwa haraka.

“Niwasihi mkamlishe zahanati hii changieni, nitaongea na halmashauri itachangia pia ili mkamilishe ujenzi huu. Haipendezi kama kwa wenzenu kijiji cha Mngoji wamejenga zahanati wamesaidiwa imekamilika, lakini mpaka leo hawajaanza kupata huduma kwa kukosa matundu mawili ya choo,” alisema Msabaha.

Said Juma mkazi wa kijiji hicho amesema: “Kweli tunahitaji huduma hali yetu sio nzuri hasa ukiwa na mgonjwa ili utoke nyumbani mpaka zahanati unatumia zaiid ya Sh2000 kwenda tu.”

Kwa mujibu wa Juma ili kupata huduma za afya, inawabidi ama kwenda mpaka kijiji cha tatu au Mtwara mjini.

“…tunafurahi kwamba sasa tutapata zahanati kwetu, ni jambo ambalo tunaamini kuwa tutasaidiwa kwakuwa tunatumia zaidi ya Sh2000 kwenda hospitali,” alisema Juma

Chanzo: mwanachidigital