Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMDA yatoa dawa, vifaa tiba magereza

IMG 4354.jpeg TMDA yatoa dawa, vifaa tiba magereza

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Mashariki imetoa msaada wa dawa za kutibu magonjwa mbalimbali pamoja na vifaa tiba zenye thamani ya zaidi ya Sh31 milioni katika Gereza Kuu la Butimba jijini Mwanza.

Akikabidhi dawa hizo Juni 21, 2023, Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Sophia Mzirayi amesema dawa na vifaa tiba hivyo zilikamatwa zikiwa sokoni kinyune na taratibu baada ya uchunguzi kuonesha ni salama kwa matumizi wakaona waiunge mkono Serikali kuhakikisha vifaa tiba vinapatikana kwenye zahanati ili wananchi wapate huduma bora.

“Dawa hizi ambazo siku ya leo tumezileta ili ziweze kuhudumia zahanati zote za magereza mkoni Mwanza ni dawa na vifaa tiba ambazo tumekuwa tukizikamata kutoka kwenye maeneo mbalimbali wakati tunafanya shuguli zetu za udhibiti,

“Zile ambazo tukizikamata kwenye soko tukazifanyia uchunguzi wa kimahabara tukagundua bado zina ubora na ni salama kwa ajili ya matumizi hizi ndizo tunakuja kuzitoa msaada kwa wenzetu ili kuunga jitihada za Serikali kuhakikisha wananchi wnapata huduma bora za afya,”amesema

Sophia amesema wana mifumo ambayo inadhibiti bidhaa hizo kabla hazijaruhusiwa kuingia sokoni ambayo ikihakikisha ubora, usalama, ufanisi na wao wakathibitisha dawa hizo ni bora, salama na zinafaa kutumika ndipo zinaruhusiwa kuingia sokoni.

“Vile vile tuna mfumo wa kuzifuatilia bidhaa hizi sokoni kuhakikisha zinaendelea kuwa na ubora ule ule, ufanisi na usalama,

“Tunatambua upande huu wa Kanda ya Ziwa tumepakana na nchi mbalimbali kuna mipaka iliyo halali na isiyo halali lakini, tunatambua bado kuna wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanataka kupata faida zaidi kwahiyo wakati mwingine wanaweza kuingiza dawa ambazo TMDA haijathibitisha ubora, usalama na ufanisi wake,”amesema

Kuhusu bidhaa zinazoingizwa nchini kwa njia ya panya na kuzikamata sokoni zikiwa bandia, duni au hazijasajiliwa, Sophia amesema bidhaa hizo zikikamatwa uteketezwa kwa moto.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Justin Kaziulaya amesema dawa hizo zitasambazwa zahanati zote za magereza mkoani humo ikiwemo ya gereza la Butimba, Magu, Ukerewe, Ngudu wilayani Kwimba na Kasungamile wilayani Sengerema.

Amesema zahanati hizo hazitibu tu askari, familia zao, mahabusu na wafungwa bali zinatibu na jamii zinaowazunguka hivyo msaada huo utanufaisha jamii nzima ya magereza huku akimtaka Mkuu wa Gereza la Butimba kuhakikisha uwiano sawa wa mgawanyo wa dawa na vifaa tiba vilivyotolewa kulingana na idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa kwenye zahanati hizo.

Ofisa Tabibu wa Zahanati ya Gereza Kuu la Butimba, Paschal Shiwala amesema msaada huo utawanufaisha wafungwa na mahabusu kati ya 600 hadi 800 na wananchi kati ya 150 hadi 200 wanaohudumiwa kwa mwezi katika zahanati hiyo.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Dk Sebastian Pima ameshukuru mamlaka hiyo akihaidi dawa hizo zitatumika kwa lengo lililokusudiwa.

Baada ya makabidhiano ya dawa na vifaa tiba, timu ya TMDA ilifanya ziara gerezani hapo na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanywa na wafungwa ikiwemo ufyatuaji matofali, ushonaji, utengezezaji viatu, kapeti pamoja na kutembelea fukwe ya ‘stress free beach resort' inayoendeshwa na Jeshi la Magereza Mkoa wa Mwanza.

Chanzo: Mwananchi