Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMA yataja sababu mvua ya mawe Biharamulo

37a38bd26bcc75e74432fe6c0e428afd TMA yataja sababu mvua ya mawe Biharamulo

Thu, 19 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mabadiliko ya hali hewa yanasababisha ongezeko la joto na matukio mengine lakini mvua yam awe iliyonyesha Biharamulo ni jambo la kawaida.

Ofisa wa Utabiri wa TMA, Rose Senyagwa alilieleza gazeti hili kuwa mvua hiyo iliyonyesha mchana Agosti 14 mwaka huu ilitosababishwa na mawingu mazito yanayojulikana kwa jina la mawingu ng’amba yanayotengeneza barafu na maji baridi.

Senyagwa alisema mawingu hayo yanaposhuka kutoka angani yakiwa katika mkusanyiko mkubwa barafu zinapodondoka zikikuta hali ya ubaridi haziyeyuki na huanguka.

“Lakini kama eneo halina hali ya ubaridi barafu hizo huyeyuka na kunyesha mvua ya kawaida hivyo siku ile Bihalamulo kulikuwa na mvua na ndiyo sababu ya kuanguka kwa barafu”alisema.

Senyagwa alisema mvua hizo si jambo geni, hutokea mara chache na zimewahi kunyesha katika maeneo ya Ziwa victoria, Manyara, Iringa na Njombe.

Alisema mvua hiyo ya mawe iliyonyesha ukubwa wa mawe ulikuwa wastani wa sentimeta 1.5 na kusababisha madhara katika mimea, mbogamboga na matunda.

Alisema lakini ikifika wastani wa sentimeta 1.9 linapofika ardhini kitaaluma linakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa binadamu na nchi.

“Ikiwa mvua hizi zitajirudia mara kwa mara tunaweza kusema ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini kwa sasa bado wataalamu wanandelea kufanya tafiti kuona kama kuna uhusiano”alisema

Akizungumzia matukio ya matetemeko na mafuriko katika maeneo mbalimbali duniani Senyagwa alisema yanasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wiki hii Tetemeko la ardhi liliua zaidi ya watu 1200 na kujeruhi wengine kadhaa nchini Haiti. Mwezi uliopita nchini China, watu wasiopungua 58 walifariki dunia kutokana na mafuriko katika mkoa wa Henan.

Alisema miaka inavyoenda mabadiliko ya tabia nchi yanazidi kuonekana na kumekuwa na tafiti mbalimbali zinazoonyesha kuongezeka kwa majanga.

Chanzo: www.habarileo.co.tz