Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMA yatahadharisha mvua kubwa kunyesha mikoa hii

MVUAAAAAA.jpeg TMA yatahadharisha mvua kubwa kunyesha mikoa hii

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamalaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia usiku wa Februari 7, 2023.

Utabiri huo umetaja maeneo yatakayokua na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Manyara.

Kwingine ni Mikoa ya Pwani ikijumuishwa na Mafia, Visiwa vya Unguja na Pemba, Mkoa wa Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Mara, Tabora, Kigoma, Katavi, Songwe, Rukwa, Mbeya na Iringa.

Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Njombe, Ruvuma, Mtwara na Lindi nayo inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo  katika maeneo machache pamoja na vipindi vifupi vya jua.

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na Mvua nyepesi katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Kwa viwango vya joto vinavyotarajiwa nchini tazama hapa chini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live