Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMA yatahadharisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe

Piii1 TMA yatahadharisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe

Thu, 18 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea kwa uharibifu wa mazao ya chakula utakaotokana na kuwepo kwa upepo mkali katika mikoa ya Ruvuma, Songwe, Mbeya na Njombe na hivyo kuwataka wakulima kuchukua tahadhari.

Meneja wa kituo cha utabiri kutoka TMA, Samwel Mbuya ameiambia EATV/EA Radio Digital kwanba upepo huo ambao sio wa kawaida pia unaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Aidha Mbuya amewataka wale wote wanaofanya shughuli zao za kiuchumi ikiwemo wavuvi katika maeneo ya baharini kuchukua tahadhari katika kipindi hiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live