Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMA yatabiri mvua kubwa mikoa tisa Tanzania

94312 Pic+mvua TMA yatabiri mvua kubwa mikoa tisa Tanzania

Mon, 3 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa leo Jumatatu Februari 3, 2020 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Ruvuma.

Taarifa iliyotolewa na TMA imesema athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Kesho Jumanne Februari 4, 2020 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa na Ruvuma.

Chanzo: mwananchi.co.tz