Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS yakabidhi msaada wa madawati Muheza

Tfs TFS yakabidhi msaada wa madawati Muheza

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Msaada huo ambao ni kwa ajili ya shule za msingi na sekondari tatu ambazo ni pamoja na ofisi za watendaji kata mbili zilizopo wilayani Muheza utasaidia kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Halima Bulembo, mhifadhi wa shamba la miti Ellyneema Mwasalanga, amesema kuwa msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia kuboresha utoaji wa huduma.

"Tumetoa viti na Meza 17 kwa ajili ya Ofisi za watendaji na madawati 60 kwa shule za msingi na Sekondari," amesema Mwasalanga.

Awali akizungumza mkuu wa wilaya ya Muheza, Halima Bulembo ameshukuru TFS kwa namna walivyothamini elimu ya watoto Wakitanzania na hivyo kwa msaada huo wataboresha utoaji wa elimu.

Halima ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kuilinda misitu na kuhakikisha hakuna uharibifu unaofanyika.

"Niwaombe wananchi huu msitu unatunufaisha hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaulinda ili uweze kutusaidia katika kukuza kipato chetu na uchumi," amesema.

Chanzo: ippmedia.com