Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS Ukerewe wagawa miche 20,000 ya miti

297578ea20a88f97fc1410b9bcb121f2 TFS Ukerewe wagawa miche 20,000 ya miti

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wilayani Ukerewe, Mwanza ikishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ukerewe inaendelea kugawa miche 20,000 ya miti katika Taasisi za Elimu pamoja na ofisi mbalimbali wilayani humo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa miche 1,200 ya miti katika Chuo cha Ualimu Murutunguru, Mhifadhi Msitu Stephen Odongo alisema miche ya miti wanayogawa ni miti ya matunda, kivuli na ya mbao.

Alisema kazi hiyo ya ugawaji miti walianza mwezi Oktoba na itafika mwisho wa mwezi Desemba mwaka huu na kuongeza kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kugawa miche 5,656 ya miti katika taasisi za pamoja na shule za msingi zikiwemo, Msozi, Myebe na Muhula.

Odongo alisema miche mingi ya miti imekuwa ikizalishwa wilayani Nyamagana kisha inapelekwa wilayani Ukerewe na kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha mazingira na kuhusisha jamii katika upandaji miti.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Maghembe aliwataka wananchi kuhakikisha wanapanda miti na kusema serikali inapata fedha nyingi sana kupitia msitu wa Rubya wenye hekari 1,926 ambao upo wilayani Ukerewe.

Alisema watatumia msitu wa Rubya kupata mbao za kutengeneza madawati 1,972 ili kumaliza kero ya madawati wilayani Ukerewe na kuwa wilaya yake inapoteza soko la kupeleka machungwa Mwanza mjini kutokana na ukataji holela wa miti ya matunda.

Chanzo: habarileo.co.tz