Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS Ukerewe kugawa miche 20,000 ya miti

23873f7a635fd93055af4ddceeb4a5a5 TFS Ukerewe kugawa miche 20,000 ya miti

Thu, 10 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) wilayani Ukerewe jijini Mwanza ikishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ukerewe inaendelea kugawa miche 20,000 ya miti mbali mbali katika Taasisi za Elimu pamoja na ofisi mbali mbali wilayani humo.

Akizungumza wakati wa kuhadhimisha kumbukumbu za siku ya Uhuru katika chuo cha Ualimu Murutunguru,Mhifadhi msitu Stephen Odongo alisema miche ya miti wanayogawa ni miti ya matunda,Kivuli na ya Mbao. Alisema zoezi hilo la ugawaji miti walianza mwezi October na litafika mwisho mwezi Desemba mwaka huu.

Alisema mpaka sasa wamefanikiwa kugawa miche 4456 ya miti katika taasisi za Serikali pamoja na shule za msingi zikiwemo,Msozi,Myebe na Muhula.Odongo alisema miche mingi ya miti imekuwa ikizalishwa wilayani Nyamagana kisha inapelekwa wilayani Ukerewe.

TFS Ukerewe pia ilitoa miti 1200 katika chuo cha ualimu Murutunguru. Odongo alisema wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) imedhamiria kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Ibara ya 68 C,''Kuimarisha ushiriki wa jamii katika usimamizi na manufaa ya rasilimali Misitu na Nyuki kwa kutekeleza programu zinazosaidia kuzalisha ajira na kipato pamoja na uhifadhi wa mazingira''.

Odongo alisema wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha Mazingira na kuhusisha jamii katika upandaji miti.Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Maghembe amewataka wananchi kuhakikisha wanapanda miti.

Alisema Serikali inapata fedha nyingi sana kupitia msitu wa Rubya wenye hekari 1926 ambao upo wilayani Ukerewe.Alisema watatumia msitu wa Rubya katika kupata Mbao za kutengeneza madawati 1972 ili kumaliza kero ya madawati wilayani Ukerewe.

Alisema wilaya yake inapoteza soko la kupeleka machungwa Mwanza mjini kutokana na changamoto ya ukataji miti katika maeneo mbali mbali wilayani humo.

Mhifadhi mkuu wa misitu pori la Rubya,Festo Chaula alisema kumekuwa na kero kubwa ya uwashaji moto ovyo unaofanywa na wavuvi wakati wa usiku.Alisema anawaomba wananchi kuhakisha wanatumia vyema pori la Rubya kwa kuwa limeleta ajira kwa wakazi wengi wilayani Ukerewe.

Chanzo: habarileo.co.tz