Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TDA yapinga agizo la RC Mtaka kuhusu "Level Seat"

34707 Usafiri+pic Usafiri

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka madereva mabasi kutokujaza abiria kwenye magari ili kuepusha msongamano wa watu.aliyasema hayo kwenye uzinduzi wa chanjo ya Covid-19 mkoa hapo, huku akionya kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watakao kwenda kinyume.

Agizo la mkuu wa mkoa wa Doodoma limewaibua wamiliki wa vyombo hivyo wakilalamika hasara iwapo agio hilo litatekelezwa. Uongozi wa chama cha Wamiliki wa Daladala TDA, Umesema kuwa watapata hasara kwa kutosimamisha abiria kwa kuwa bei ya mafuta imepanda.

Malalamiko hayo yameibuka wakati Mtaka akitoa agizo hilo,ikiwa ni hatua ya kupambana na kusamba kwa virusi vya corona, ambapo ameagiza mabasi ya abiria yanayofanya safari zake za ndani ya mkoa huo,daladala,bodaboda kubeba abiria kulingana na uwezo wa chombo husika.

Hata hivyo,toka Mtaka ametoa agizo hilo ni bado utekelezaji wake umekwama,daladala zimendelea kujaza abiria,bajaji zinajaza na bodaboda zimendelea kubeba mshikaki kama kawaida.

Kiongozi wa TDA Hamisi Mnyakongio akizungumza na wanahabari alisema, hawawezi kutekeleza kwasababu bei ya mafuta imepanda,huku viwango vya nauli vikibaki vilevile hii itakuwa hasara kwetu.

Alisema licha ya namaumivu ya mafuta kupanda,bado kiwango cha nauli ha daladala kwa njia ya mahesabu wanazotakiwa kuwakilisha kwa mabosi zao kipo palepale hali inayofanya wafanye kazi katika mazingira magumu.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma ,Onesmo Lyanga alisema ikiwa wana malalamiko kuhusu tamko hilo wanatakiwa wamfamte Mtaka kwa majadiliano,na kama watakwenda kinyume na agizo sheria itachukua mkondo wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live