Arusha. Mamlaka ya usimamizi wanyamapori (TAWA) imetangaza mkakati wa kuwalinda Flamingo wa eneo la Ramsar Ziwa Natron, lililopo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha kwa kutaka eneo hilo kupandishwa hadhi kutoka ardhi owevu kuwa Pori la Akiba.
Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko amesema eneo hilo la ziwa Natroni ni la kipekee duniani hivyo kuhitaji kutunzwa na kulindwa ili Flamingo waendee kuwepo.
"Lakini ni wajibu wa TAWA kupanga mikakati ya kuona utalii katika eneo hili unaongezeka na kuleta mapato zaidi yatakayowanufaisha wananchi wanaozunguka eneo hili Watanzania, TAWA na Serikali kwa ujumla" amesema.
Amesema wanataka kulipandisha hadhi eneo hilo kutoka kuwa Pori Tengefu (Game Controlled Area) kuwa Pori la Akiba (Game Reserve).
“Tunatarajia yatafanyika kwa maridhiano kati yet una Vijiji vinavyozunguka eneo hili la Ziwa Natron, ili kurahisisha mchakato huu” amesema
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi TAWA Dk. James Wakibara amesema ndege aina ya Flamingo wanaozaliana Ziwa Natron ni maarufu duniani kutokana na maisha yao kuzingatia mahitaji nyeti.
Pia Soma
- Bashe: Siikosoi Serikali kwa sababu ya Lowassa - VIDEO
- Dk Ndugulile: Wafundisheni wananchi umuhimu wa kuacha wosia
- Miaka 10 Kikoba cha Juhudi care, mtaji wakua mara 5 zaidi
“Inategemea duniani hiyo Kemia iko wapi,katika hili Kemia ipo Ziwa Natron ndipo tunaposema lina sifa ya kipekee duniani, kwani utakwenda kila mahali lakini ukimaliza ziwa hili Flamigo watatoweka duniani,