Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAF yatenga Sh24.3 bilioni kutekeleza miradi Njombe

Fedha Wagawana TASAF yatenga Sh24.3 bilioni kutekeleza miradi Njombe

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini (TASAF) umetenga Sh24.3 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya awamu ya nne ya kupunguza umasikini mkoani Njombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema hayo wakati wa kikao kazi kilichofanyika mkoani humo na kusema kuwa fedha hizo zitasaidia kupunguza changangamoto zilizopo za miundo mbinu.

Amesisitiza kufuata utaratibu wa kisheria katika matumizi ya fedha hizo.

"Kitu kikubwa kuhakikisha kwamba tunatekeleza miradi ambayo ndiyo uhitaji halisi wa wananchi katika maeneo yao" amesema Mwamanga.

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Mhandisi Marwa Rubirya amewataka wataalam na wasimamizi wa miradi hiyo kufuata weledi na uadilifu katika majukumu yao.

Amesema uongozi wa mkoa na wilaya hautawavumilia watendaji ambao watajihusisha na vitendo vya kuhujumu miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Meneja miradi wa Tasaf, Paul Kijazi amesema katika miradi iliyopita yapo mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya na elimu hasa katika ujenzi wa madarasa na vituo vya afya na zahanati.

Chanzo: mwananchidigital