Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TARURA YAKAMILISHA BARABARA KM 6.2

58a1ab5d0a9220cce7cb872736230889 TARURA YAKAMILISHA BARABARA KM 6.2

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imesema tayari imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 6.2 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.1 na kilomita zingine 1.8 zipo katika mchakato wa matengenezo.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TARURA katika halmashauri hiyo, Mhandisi Lusekelo Mwakyami alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi wilayani humo.

Aidha, Mhandisi Mwakyami amesema kuwa ujenzi huo unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia mpango wa kuziwezesha halmashauri mbalimbali hapa nchini kwenye kuboresha miundombinu ya barabara ambapo kwa sasa unasimamiwa na TARURA.

“Tunatekeleza miradi yetu kwa kulenga maeneo ya kiuchumi na kijamii kama vile vituo vya afya, shule na maeneo ya biashara ili kuboresha mazingira ya kuishi na kukuza uchumi wa wananchi” amesema Mhandisi Mwakyami.

Chanzo: habarileo.co.tz