Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TARI Naliendele wafikia tamati ugonjwa wa mnyauko

9c082be3f944f2abd3602d30bb560923.png TARI Naliendele wafikia tamati ugonjwa wa mnyauko

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KITUO cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele kiko katika hatua za mwisho za kukamilisha ufumbuzi wa ugonjwa wa mnyauko ambao kwa sasa unaleta shida katika ukuaji wa zao la korosho nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tari, Dk Geofrey Mkamilo aliyasema hayo wakati wa kikao cha kutathmini kazi ambazo kituo cha Naliendele kilitekeleza kwa kipindi cha mwaka 2019/2020.

"Ugonjwa wa mnyauko tuna matokeo kabisa ya awali ambayo tunaridhika nayo na ndani ya mwaka mmoja mpaka mwaka mmoja na nusu tutakuwa tayari tuna uvumbuzi wa ugonjwa huo ambao ni ugonjwa mpya unaoleta shida kidogo tofauti na magonjwa mengine ambayo tuliyazoea," alisema.

Dk Mkamilo alisisitiza kuwa tayari kituo hicho kimeshapata matokeo ya awali na kuwaeleza watendaji wa halmashauri mbalimbali nchini na kuwa uelewa kuhusu hatua zilizofikiwa na kituo hicho katika kutatua tatizo.

Katika hatua nyingine, Dk Mkamilo alisema TARI pia wako katika hatua za kukamilisha na kutoa mbolea ambayo itasaidia kuongeza uzalishaji wa zao la korosho.

Alisema mbolea hiyo ambayo ni ya kupulizia kwenye majani badala ya kupulizia chini ya miti ya korosho inatakiwa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la korosho kwa wingi.

"Tumetoa uelewa kwenye matumizi ya mbolea kwenye zao la korosho, mbolea hiyo ni ya kupulizia kwenye majani na tayari kuna matokeo ambayo ni mazuri tunayotarajia kwa ajili kuongeza uzalishaji wa korosho hasa kwa ajili ya matumiz ya mbolea,"alisema.

Pia Dk Mkamilo alisema kwamba kituo hicho kinatafiti ili kuleta matumizi ya viua magugu ambavyo vitatumika badala ya kutumia jembe la mkono katika kupalilia mikorosho.

"Tunataka pia kuwapunguzia wakulima wetu hasa akinamama na vijana kuacha kutumia muda mwingi wa kukaa shambani, tutakuja kuwaeleza jinsi ya kutumia viuagugu ndani ya mwaka mmoja au miwili tutakuwa tunawaleza kwamba sasa badala ya kutumia jembe la mkono waendelee kutumia viua gugu," alisema.

Wakati huo huo Dk Mkamilo alisema kituo cha TARI Naliendele kinatarajia kupata tani 100 za mbegu bora za korosho na kuziuza kwa wakulima katika maeneo yote ambayo yanalimwa zao la korosho.

Chanzo: habarileo.co.tz