Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANROADS Morogoro yajivunia ubora mtandao wa barabara

TANROADS Morogoro Yajivunia Ubora Mtandao Wa Barabara.jpeg TANROADS Morogoro yajivunia ubora mtandao wa barabara

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro inajivunia ubora wa mtandao wa barabara zake unaofika kilomita 2,071.23 zinazopitika mwaka mzima.

Meneja TANROADS Morogoro Mhandisi Lazeck Kyamba mbali ya kuridhishwa na ubora wa mtandao wa barabara hizo, amesema wakala umeendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa mtandao huo wa barabara unakuwa bora muda wote.

"Tupo vizuri ukizingatia kuwa sisi (morogoro) ndi langu kuu la uchumi kwa taifa na kuimarika kwa barabara kunachochea maemdeleo ya kiuchumi na kijamii kwa ujumla wake,’’ alisema mhandisi Kyamba’’.

Kwa mujibu wa meneja huyo mkoa, katika mtandao huo katika barabara kuu (trunk roads) kuna kilomita 849.42 kati ya kilomita hizo kilomita 464.87 ni za changarawe na kilomita 384.55 ni lami.

"Kwa upande wa barabara za mkoa (regional roads) tuna kilomita 1,221.81 kati ya mtandao huo wa barabara kilomita 1,054.31 ni lami wakati kilomita 167.50 ni za changarawe,’’ alisema mhandisi Kyamba

Mhandisi Kyamba alisema kuwa mtandao wa barabara kuu upo vizuri ikiwemo daraja la kiyegeya ambalo ni kiungo muhimu sana kati ya mkoa wa Morogoro na mikoa ya nyanda ya kati ya Tanzania.

"Ofisi inatunza na kusimamia vituo vitatu vya mizani vya Mikese, Dakawa na Mikumi. Tunatoa rai pia kwa wasafirishaji wa mizigo na abiria kuhakikisha magari yao yanabeba mizigo kulingana na viwango vya uzito vinavyo ruhusiwa kisheria’’ alisema

Mhandisi Kyamba ambaye alikuwa akiongea na waandishi wa habari wanaofuatilia maendeleo na ustawi wa barabra mkoani hapa kwa niaba ya mtendaji mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta alisema serikali ya awamu ya sita imeazimia kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya ujenzi wa barabra nchini.

‘’Tumeendelea kutekeleza maagizo na maelekezo ya viongozi wetu mbalimbali wa chama na serikali katika ngazi mkoa na kitaifa . Maelekezo kuhusu vivuko na alama za barabarani yamekuwa yakitekelezwa,’’ alisema na kutolea mifano Mikese eneo la Gezaulole, Mkundi stendi , Bingwa, Masika, Mkambarani, Gairo na Kihonda.

Mhandisi kyamba alisema wakala mkoami humo imejipanga kufikia malengo ya serikali ya awamu ya sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live