Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANROAD wakanusha kuharibika kwa uwanja wa ndege Chato

Tanroads Pc Data TANROAD wakanusha kuharibika kwa uwanja wa ndege Chato

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Geita imekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha uwanja wa ndege wa Geita ukiwa na mipasuko na nyasi, ikisema ni za uzushi na zenye lengo la kuhujumu uwanja huo.

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi wa njia za ndege, Meneja wa Tanroads mkoani hapa, Haruna Senkuku amesema uwanja huo upo kwenye hali ya ubora na ndege zinatua mara tatu kwa wiki.

“Ndege ziko kwenye viwango vya juu vya ubora na umehakikiwa na mashirika yote yanayohusika na viwanja vya ndege uwanja huu unatumiwa na ndege za ndani na nje kama mtakumbuka wamewahi kutua marais kutoka Kenya, Uganda na Msumbiji na wikiijayo tunategemea kupewa leseni ya moja kwa moja ya uwanja,” amesema Senkuku.

Ofisa usalama uwanja huo, Hellen Osoro amesema uwanja huo hutumika kila siku za jumatatu, Alhamisi na jumamosi kwa ndege za abiria za shirika la ndege la ATCL.

Uwanja wa ndege Geita ulijengwa na mkandarasi wa ndani ambae ni Mayanga Constraction chini ya usimamizi wa wakala wa barabara mkoani hapa kwa gharama ya Sh 58 bilioni ambazo ni fedha za ndani.

Chanzo: mwananchidigital