Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO yatoa tahadhari kukosekana huduma ya umeme Dar

Umeme Tanesco TANESCO yatoa tahadhari kukosekana huduma ya umeme Dar

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema linaendelea kuhakikisha kuwa upatikanaji wa huduma ya umeme ni ya uhakika na wa kutosha muda wote na ili kufanikisha hilo, Shirika limepanga kufanya matengenezo ya mtambo namba mbili (2) wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wa Songas uliopata hitilafu.

“Matengenezo haya yanafanyika leo Jumatatu, tarehe 24 Oktoba 2022 kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 8 mchana, iwapo matengenezo kwenye mtambo huu yatachelewa kufanyika, itasababisha madhara makubwa kwenye mtambo husika, hali itakayosababisha athari za upatikanaji umeme kwa muda mrefu”

“Wakati wa matengenezo haya, baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam yataathirika kwa kukosa umeme, aidha Wateha wa maeneo yote yatakayoathirika watatumiwa SMS kwenye simu zao, Shirika linawashukuru Wateja wote kwa ushirikiano mtakaouonesha kipindi chote cha matengenezo haya”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live