Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO yaahidi huduma bora Kanda ya Ziwa

775a837ac355ba66fa54c25af6fd408f TANESCO yaahidi huduma bora Kanda ya Ziwa

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKA la Umeme nchini(TANESCO) limeungana na watoa huduma mbalimbali katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa wateja huku ikiahidi kutoa huduma bora zaidi.

Akizungumza wakati maadhimisho hayo meneja mwandamizi wa shirika hilo Kanda ya Ziwa, mhandisi Henryfried Byabato amesema shirika hilo lina kazi kubwa ya hukakikisha kuhudumia wateja wake.

‘’ Tuna kazi kubwa sana ya kuhudumia wateja wetu haswa walioomba umeme haswa baada ya punguzo la bei ya Tsh 27,000/-‘’ amesema mhandisi Byabato.

Amesema wanaendelea na mikakati ya kuhakikisha wateja wao wanapata umeme pamoja na kukarabati ipasavyo miundombinu ya umeme.

‘’Baada ya kupunguza bei wateja wameongezeka sana katika mkoa wa Mwanza,fomu za maombi kwa mwezi zilikuwa 1500 lakini kwa sasa wateja wanaomba maombi ya kuwekewa umeme ni 6000’’ ameongeza mhandisi Byabato.

Afisa uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Mwanza, Flaviana Moshi amesema watatumia wiki ya huduma kwa wateja kutoa elimu ya usalama kwa matumizi ya umeme kutokana na wateja wengi wanatumia umeme kwa mazoea.

Amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa baadhi ya watu kufanya biashara katika miundombinu ya umeme kama Transfoma na nguzo za umeme.

Moshi amesema wanapata changamoto ya uharibifu wa miundo mbinu kutoka kwa wakulima haswa wanapokuwa wanaanda mashamba yao wamekuwa wakichoma miundo yao ikiwemo nguzo na nyaya za umeme.

Kaimu meneja Tanesco, Mkoa wa Mwanza, James Kabasa amesema kwa mkoa huo mpaka sasa wana wateja 166,903. Amesema wanajipanga kuhakikisha wateja wao wanapata umeme na shirika lao litaendelea kuboresha huduma zao.

Chanzo: www.habarileo.co.tz