Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO mkizingua tutazinguana - RC Mndeme

MNDEME WEB 660x400.jpeg TANESCO mkizingua tutazinguana - RC Mndeme

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Christina Mndeme ameitaka TANESCO mkoa huo kutokuwa chanzo cha kikwazo cha wananchi kupata maji safi na salama baada ya mradi wa muda mrefu ambao upo katika halmashauli ya Madaba kukamilika.

Amesema mradi huo umekamilika lakini kikwazo kipo katika shirika hilo kupeleka umeme ili wananchi wa Halmashauli hiyo waondokane na kero kubwa ya maji ambayo wanaipata.

”Nataka Alhamisi wiki ijayo maji yaanze kutoka, TANESCO mkinizingua tutazinguana, na atakayenikwamisha awe TANESCO au RUWASA ama mtu yeyote mwenye nia mbaya Tutazinguana,”  Mndeme.

Mradi huo wa maji upo katika Halmashauri ya Madaba iliyopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma na serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.

DC SABAYA AKUTA MAFUTA LITA TANO YANAUZWA ELFU 34, AKASIRIKA AMBANA MFANYABIASHARA “TUTAZINGUANA”

Chanzo: millardayo.com