Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO kuokoa Bilioni 1 Ngorongoro

Tanesco.jpeg Wilaya ya Ngorongoro ilikuwa ikitumia umeme wa jenereta

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (Tanesco), imekamilisha ujenzi wa mradi wa umeme wenye thamani ya Sh2.9 bilioni wa kuiunganisha Wilaya ya Ngorongoro kwenye grid ya taifa.

Awali, Wilaya ya Ngorongoro ilikuwa ikitumia umeme wa jenereta ambao ulikuwa ukigharimu Sh1.7 bilioni zikiwa ni gharama za uendeshaji kwa mwaka, huku makusanyo ya wilaya ya Ngorongo yakiwa ni Sh374 milioni kwa mwaka.

Akizindua umeme huo wa gridi katika Wilaya ya Ngorongoro katika Halmashauri ya mji mdogo wa Loriondo jana, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela alisema Tanesco imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuwafikishia huduma ya umeme wananchi sambamba na kuboresha miundombinu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live