Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANESCO kukomesha kukatika hovyo kwa umeme

MD  1 Kituo kimekua kikipata hitilafu za mara kwa mara

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la umeme nchini (TANESCO) limesema limejipanga kumaliza changamoto ya hitilafu inayojitokeza mara kwa mara katika kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Msamvu (Msamvu Substation) mkoani Morogoro kwa kununua vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kubaini hitilafu kabla haijatokea na kuathiri miundombinu ya Shirika hilo.

Akizungumza Mjini Morogoro mara baada ya kutembelea na kujionea kazi zinazofanywa na mafundi wa TANESCO katika kituo cha Msamvu za kuhakikisha hali ya upatikanaji wa umeme inaimalika mkoani Morogoro na maeneo ya jirani kutokana na kuungua kwa kituo hicho Mkurugenzi wa TANESCO Bwana.

Mharage Chande amesema shirika litaongeza vitendea kazi na tayari shirika hilo limeanza kufanya tathimini ghalama ya kufanya matengenezo ya mashine umba (Transfoma ) kubwa zote nchini ili kuona ni kiasi gani kitatumika katika kufanya matengenezo.

Amesema kutokana na Mkoa wa Morogoro kuwa tegemezi katika uzarishaji wa mazao ya chakula na biasharana pamoja na uwepo wa viwanda kumeufanya Mkoa kuwa na matumizi makubwa ya nishati ya umeme hivyo TANESCO ipo katika mpango wa kuongeza kituo kingine cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme ambacho kitakuwa kikubwa zaidi.

Aidha amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuacha kupeana lawama kufuatia matukio ya kuungua kwa kituo cha Msamvu badala yake wafanye kazi na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora ya nishati ya umeme.

Kwaupande wake msemaji wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Martin Mwambene amesema kazi ya kusafirisha mashine umba (Transfoma) kutoka kwenye kituo cha Zuzu mkoani Dodoma mpaka Msamvu limekamilika na kinachendelea ni zoezi la kuifunga Transfoma hiyo ambapo amsema kazi ya kufunga Transfoma itakamilika hivi karibuni.

PIA amesema kuungua kwa kituo cha Msamvu kumesababisha mikoa ya Kaskazini kukosa umeme wa uhakika kutokana na kuzidiwa kwa njia za kusafirishia umeme katika kituo cha Chalinze ambacho awali kilikuwa kinatumika kusafirisha umeme wa mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro huku akiwatoa hofu wakazi wa maeneo hayo kuwa nishati hiyo itarudi katika hali ya kawaida baada ya kukamilika kwa matengenezo katika kituo cha Msamvu.

Ikumbukwe kuwa Agost 2, 2021, Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Msamvu mkoani Morogoro kilipata hitilafu iliyosababisha kuwaka moto kwa jumba la kudhibiti mifumo ya umeme wa msongo wa kilovolti 33.

Aliyekuwa Wziri wa Nishati Dk Kalemani aliagiza kuwasimamisha kazi watumishi watatu wa Shirika hilo mkoani Morogoro wakipisha uchunguzi utakapomalizika ambao uchunguzi huo pia unamhusisha na mfanyakazi mwingine mmoja wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Mwendokasi (SGR).

Licha ya kuchukua hatua hizo pia alitembelea eneo Tungi, Manispaa ya Morogoro ilipo kebo ya umeme ambapo inapodaiwa ni chanzo cha kuungua moto jengo la mitambo katika kituo hicho.

Ni kutokana na kukatwa kwa bomba lenye kebo iliyochimbiwa chini ya ardhi ambayo inaunganika na kituo hicho kufuatia mtambo wa kuchonga barabara (Burudoza) ya kampuni ya Yapi Merkezi iliyojenga reli ya mwendo kasi(SGR) kukatwa kwa kebo hiyo .

Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati , moto huo umesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili na kukosekana kwa huduma ya umeme wa uhakika mkoani humo.

Kufuatia tukio hilo , Augosti 14, 2021 , Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Tanzania Kassim Majaliwa, alipotembeela kituo hicho aliuangiza Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufanya mapitio ya wataalamu wote wanaosimamia vituo 51 vya kupokea na kupoza umeme nchini.

Alisema lengo ni kuona kama wanakidhi vigezo na kuona kama wanafanya kazi kwa weledi kutokana na kusimamia mitambo hatari .

Pia tukio la pili lilitokea Aprili 13, 2022 kwa mashine umba (Transfoma ) iliyoko kwenye Kituo cha Kupokea na kupooza umeme cha Msamvu kuungua moto na kusababisha sehemu kubwa ya amkoa wa Morogoro na mikoa jirani kukosa huduma ya umeme .

Licha ya maeneo ya wilaya za mkoa huo pia kuungua kwa mashine umba hiyo kulisababisha mikoa Jirani ikiwemo Pwani , mikoa ya kanda ya Kaskazini na Dar es Salaam iliathiriwa.

Kwa mujibu wa uongozi wa Taneseco kwa sasa kunavituo 51 vya kupokea na kupoza umeme Nchi nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live