Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU yafanikiwa kufuatilia miradi ya Bil. 10.2 Kinondoni

TAKUKURU Yafanikiwa Kufuatilia Miradi Ya Bil. 10.2 Kinondoni TAKUKURU yafanikiwa kufuatilia miradi ya Bil. 10.2 Kinondoni

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni imefanikiwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo yenye thamani Sh 10, 221, 000,000 na kuchukua hatua mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23/2/2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utekelezaji kuanzia Oktoba hadi Disemba 2022, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Bw. Ismail Seleman, amesema kuwa miradi hiyo ni ujenzi wa madarasa 10 katika Shule ya Sekondari Kondo – Kunduchi wenye thamani wa Sh 441,000,000.

Bw. Seleman amesema kuwa katika kufatilia mradi wa ujenzi wa madarasa walibaini kuendelea kwa ujenzi bila fundi Mkuu wala msimamizi wake hali iliyopelekea Mkuu wa Shule kuwa anasimamia mafundi.

“Hatua iliyochukuliwa Afisa Elimu Wilaya alimsimamisha fundi huyo na kuagiza utumike utaratibu wa Petty Cash kumaliza ujenzi wa madarasa hayo, baada ya hatua hizo mradi umekamilika na madarasa yameanza kutumika” amesema Bw. Seleman.

Ameeleza kuwa maradi mwengine ni ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mwenge wenye thamani ya Sh. 9,810,000.81 ambapo baada ya kufatilia walibaini kuwepo kwa ucheleweshaji wa muda wa kukamilika kwa mradi jambo ambalo limesababishwa na kizuizi kinachotokana na kuwepo kwa majengo ya watu binafsi ndani ya eneo la mradi ambapo mkandarasi ana shindwa kutekeleza mradi kwa wakati.

- Advertisement - Bw. Seleman amesema hadi ufuatiliaji umefanyika mradi umetekelezwa kwa 77% na mkandarasi alikua ameshalipwa

20.75 ya malipo.

Katika hatua nyengine amebainisha kuwa wamepokea jumla ya taarifa 78, kati ya hizo taarifa zinazohusu vitendo vya Rushwa zilikuwa 40 na zisizohusu masuala ya Rushwa ni 38.

- Advertisement - Amesema taarifa ambazo zilizohusu rushwa wamefanikiwa kufungua majalada ya uchunguzi na yanaendelea na uchunguzi na manne yamekamilika na kwenda katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, huku malalamiko 38 watoa taarifa walielimishwa na kushauriwa namna bora ya kushughulikia.

Hata hivyo amesema kuwa wamefanya uchambuzi wa mfumo wa uendeshaji wa masoko ya biashara katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ili kufanya tathmini ya uendeshaji wa masoko ya biashara, kufatilia usimamizi wa mapato yatokanayo na tozo, kodi na ushuru wa masoko na kubaini mambo mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara kuwa kizimba zaidi ya kimoja na kuvipangisha kwa bei ya juu kuliko Ile ya Serikali.

Ameeleza kuwa pia wamefanikiwa kufungua kesi saba katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na kufanya jumla ya kesi zinazoendelea mahakamani kuwa 24, huku akibainisha kuwa kesi tatu zilitolewa hukumu na Jamhuri ilipata ushindi wa kesi mbili.

Bw. Seleman amesema kuwa ili kuhakikisha TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni inatoa huduma inayowafikia wananchi wote, wamezindua programu ya Takukuru – Rafiki.

“Programu hii imelenga kuongeza wigo wa kuwashirikisha wananchi na wadau katika kutambua na kutatua kero katika utoaji wa huduma ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kero ambazo zikiachwa pasipo kutatuliwa au kupatiwa ufumbuzi zinazoweza kusababisha kutokea kwa vitendo vya rushwa kwenye jamii” amesema Bw. Seleman.

Hata hivyo ametoa wito wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na pia kuepuka matapeli wanaoibuka na kuwapigia simu kwa kuwatisha kuwa wana tuhuma zao hivyo kuwadai pesa ili waweze kuzifuta tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live