Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU yabaini mapungufu miradi 9 Rukwa

TAKUKURU Yabaini Mapungufu Miradi 9 Rukwa.jpeg TAKUKURU yabaini mapungufu miradi 9 Rukwa

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa, Mkoani Rukwa imefuatilia na kuchunguza miradi tisa ya ujenzi yenye thamani ya shilingi Milionii 836 kwa lengo la kujua thamani kama inalingana na utekelezaji wake.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wa mkoa wa Rukwa THOMAS MSUTA amesema ufuatiliaji huo umefanyika katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi April hadi mwezi June mwaka 2023, na kubaini mapungufu katika miradi sita kati ya tisa.

MSUTA amesema miradi hiyo ni pamoja na miradi mitatu ya ujenzi wa miundombinu ya shule yenye thamani ya shilingi milioni Zaidi ya 200 na miradi mingine ni miundombinu ya barabara na ujenzi wa zahanati katika vijijii vitatu mkoani Rukwa.

Amesema pamoja na kubaini mapungufu katika utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ya wananchi, lakini pia wameshauri kuongezeka kwa kasi ya utekelezaji wa miradi kwenda na muda uliopangwa kwenye mikataba ya ujenzi.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Rukwa wameishukuru TAKUKURU kwa ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi, vinginevyo miradi mingiu isingweza kukamilika kwa wakati, isipokuwa msukumo wa TAKUKURU umetoa mchango kukamilika kwa kufuata thamani ya fedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live