Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TAKUKURU wabaini madudu miradi Ilala

Rushwasssddddccc.png TAKUKURU wabaini madudu miradi Ilala

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ilala imebaini ukiukwaji wa mikataba, taratibu za manunuzi pamoja na matumizi kutoendana na malengo katika miradi ya maendeleo iliyokaguliwa ikijumuisha sekta za afya, ujenzi, elimu na huduma za jamii.

Taarifa ya ukaguzi ya robo mwaka kuhusu miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 15 iliyotolewa leo Mei 23, 2023 jijini Dar-es-salaam na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Sosthenes Kibwengo imeonesha dosari katika miradi mitatu kati ya sita.

"Kupitia ufuatiliaji huu, miradi mitatu yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4 ilionekana na mapungufu ikiwemo ujenzi wa maliwato (30) ya Umma Mkoa wa Dar-es-salaam unaotekelezwa na DAWASA yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 3, ujenzi wa kituo cha Afya Segerea wenye thamani ya Sh milioni 500, sambamba na mradi wa utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yenye thamani ya zaidi ya Sh

Chanzo: www.tanzaniaweb.live