Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sungusungu watakiwa kudhibiti uhalifu

Sungusungu.jpeg Sungusungu watakiwa kudhibiti uhalifu

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Jeshi la Jadi Sungusungu Manispaa ya Shinyanga limetakiwa kuimarisha ulinzi ili kudhibiti vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao yakiwemo matukio ya watu kushambuliwa kwa mapanga na visu pamoja na kuwafichua wanaojihusisha na mitandao ya uhalifu ili kukomesha vitendo huvyo.

Akizungumza na viongozi wa Jeshi la Jadi Sungusungu Tarafa ya Shinyanga Mjini,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amesema yamekuwa yakitokea matukio ya uhalifu ikiwemo watu kukatwa mapanga na kuchomwa visu huku jeshi la sungusungu lipo maeneo hayo na kuwataka kuwa wakali ili kukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake Kamanda Mkuu wa Sungusungu Manispaa ya Shinyanga John Kadama amesema wamejipanga kuhakikisha wanakomesha matukio ya uhalifu.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakaeleza namna ambavyo watakwenda kudhibi matukio ya uhalifu kwenye maeneo yao.

 

Chanzo: eatv.tv