Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sugu amuomba JPM atembelee Mbeya

34962 Mbilinyi+pic Mbunge Joseph Mbilinyi SUGU

Mon, 7 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema anatamani Rais John Magufuli afanye ziara mkoani Mbeya kabla muda wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 haujakaribia.

 

Amesema anaamini ujio wake utakuwa na faida kubwa kwa maendeleo ya wananchi wa Mbeya.

 

Sugu alibainisha hilo jana wakati akiunga hoja ya mkazi wa Mabatini jijini hapa, Zubeiry Shaban, ambaye alimwagiza mbunge huyo kumfikishia ujumbe Rais Magufuli kwamba Mbeya kuna watu ambao walimpigia kura, hivyo wanatamani kumueleza kero zao.

 

Sugu alifika katika Shule ya Msingi Mabatini kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo na ndipo akatoa nafasi kwa wananchi kumuuliza maswali na kutoa mapendekezo juu ya maendeleo kwa jiji hilo.

 

Shabani alisema, “Tunaomba unapofika bungeni umwambie mheshimiwa Rais kwamba na huku kuna watu wa kuongea naye kama wana Mbeya tuna kero nyingi za kumueleza, ahsante.”

 

Baada ya maelezo hayo, Sugu alisema hata yeye katika mikutano yake mingi amekuwa akiomba Rais Magufuli afike Mbeya kwani ni Rais wa wote na ujio wake utakuwa na faida kubwa katika kusukuma maendeleo ya Jiji la Mbeya na mkoa kwa ujumla.

 

“Hata mimi kwa kweli nataka sana Rais aje Mbeya na katika mikutano yangu mingi ya hadhara nimeomba Rais aje atembelee na Mbeya pia kwa sababu akichelewa sana watasema anakuja kwa vile muda wa uchaguzi umekaribia.”

 

Alisema kuwa: “Kwa hiyo hata mimi nataka Rais aje kwa sababu sisi wana Mbeya zipo ahadi alizotoa wakati wa kampeni 2015. Alituahidi kwamba akishinda atatusaidia maendeleo ikiwamo barabara ile ya Mapelele ambayo imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi.”

 

Sugu alisema amaamini hata watendaji wake wakisikia Rais anakuja Mbeyam basi wataanza kutekeleza baadhi ya mambo kwa haraka, hivyo ujio wake una faida nyingi kwa Mbeya kwani ni Rais wa wote.



Chanzo: mwananchi.co.tz