Stendi Kuu ya kisasa ya Mabasi Nyegezi, hii leo Juni 5, 2023 imeanza kutoa huduma ya usafiri wa mabasi kwenda Mikoa mbalimbali nchini, ambayo ujenzi wake umegharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi 15 Bilioni huku baadhi ya weneyji wa Mkoa huo wakifurahia kuanza kwa huduma.
Stendi hiyo, ina uwezo wa kuingiza Mabasi 120 kwa wakati mmoja, maegesho ya magari madogo 80 na ndani yake kuna huduma za Kibenki, Migahawa, Supermarket, jengo la abiria, Maduka makubwa 44, na sehemu ya vyoo.
Wamesema, ndani ya Stendi hiyo kuna chumba maalumu kwa ajili ya akina mama kunyonyesha watoto pindi wawapo safarini na kufanya upekee wa jambo hilo ambalo halipatokani katika maeneo mengine ya vituo vya usafiri wa mabasi nchini kitu ambacho kimewafurahisha.
Aidha, wameongeza kuwa, kukamilika kwa Stendi hiyo pia kutatoa nafasi kwao na Wafanyabiashara waliokuwepo kabla ya ujenzi kupatiwa vyumba vya biashara, kama alivyoagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake Jijini Mwanza Oktober 17, 2022.