Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Songwe kuanzisha utalii wa utamaduni

10449 GALAWA+PIC TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songwe. Mkoa wa Songwe unatarajia kuanzisha utalii wa utamaduni na vivutio vingine vilivyopo mkoani humo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Juni 30, 2018 na mkuu wa mkoa huo, Chiku Galawa katika maadhimisho ya siku ya Kimondo yanayofanyika katika kijiji cha Ndolezi.

Galawa amesema sambamba na vivutio vya utalii vilivyopo, pia mkoa huo unatarajia kufanya utalii wa utamaduni wa jadi, shughuli za wakazi wa mkoa huo ikiwemo kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

Galawa amesema lengo la kufanya utamaduni huo ni kuongeza vivutio vya utalii wenye lengo la kuongeza pato la wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Waziri Maliasili na Utalii,  Japhet Hasunga amewatala Watanzania kutembea kifua mbele kijivunia kwa kuwa nchi yeo ina kila kitu kinachowafanya watembeee kifua mbele.

Amesema wizara hiyo imebuni kuanzisha maonyesho ya utamaduni ambayo yatafanyika kila mwaka kuanzia Septemba hadi Septemba 31

Chanzo: mwananchi.co.tz