Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Songwe, Ruvuma zaongoza mimba za utotoni

Mimba Wanafuzi Songwe, Ruvuma zaongoza mimba za utotoni

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto ya Mwaka 2022, Mkoa wa Songwe unaongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ukilinganisha na mikoa mingine ya Tanzania.

Rais Dkt. Samiam Suluhu Hassan amesema hayo wakati akizindua ripoti hiyo na ugawaji wa magari ya kubebea wagonjwa na vifaa tiba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema “sote tunao wajibu wa kulinda maisha ya watoto wetu tutimize wajibu wetu, ripoti hii inaonesha kumekuwa na mafanikio katika kupunguza mimba za utotoni, kutoka 27% mwaka 2015/2016 hadi 22% mwaka 2022. tumepunguza kwa 5%.”

“Tumeona mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Shinyanga imepunguza kiwango cha mimba za utotoni kwa kasi kubwa zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine hili ni jambo zuri na la kupongezwa hongereni kwa mikoa hiyo.”

“Mikoa inayoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mimba za utotoni ni Songwe (45%), Ruvuma (37%), Katavi (34%), Mara (31%) na Rukwa (30%).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live