Soko la Manzese lililopo katika Halmashauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe limeteketea kwa moto, ulioanza Majira ya saa 12 asubuhi leo novemba 16.
Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kuuzima moto huo, Mpaka sasa Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
Aidha inaelezwa kuwa jumla ya maduka 33 katika Soko hilo yameteketea kwa moto.
Nae Mkuu wa wilaya ya Momba Fakii Lulandala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati wa zoezi la kuzima moto.
Lulandala amesema jengo lililokuwa na maduka 43 lote limeungua ambapo katika hayo, maduka 10 yalikuwa hayana kitu na 33 yalikuwa na bidhaa.
Aidha Lulandala amesema chanzo cha moto hadi sasa hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea.
Endelea kufatilia TanzaniaWeb kwa taarifa zaidi.