Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita wanusurika kifo gesti ikiteketea moto Arusha

Gest Pic Data Sita wanusurika kifo gesti ikiteketea moto Arusha

Sun, 16 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Watu sita wamenusurika kifo baada ya nyumba ya kulala wageni ‘gesti’ iliyopo Maji ya Chai wilayani Arumeru mkoani Arusha kuteketea kwa moto wakiwa wamelala.

Moto huo uliotokea ghafla wakati watu hao wakiwa wamelala unadaiwa kusababishwa na mtu mmoja ambaye alitoweka baada ya moto huo ukiunguza gesti hiyo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili Januari 16, 2022 mmiliki wa gesti hiyo ambaye ni miongoni mwa walionusurika, Silvester Masawe amesema tukio hilo limetokea Ijumaa alfajiri wakati yeye pamoja na wateja wake watano wakiwa wamelala.

"Kwa kweli hakuna kilichookolewa kila kitu kimeteketea kwa moto zikiwemo nguo za wageni na thamani ya mali zilizoungua pamoja na jengo inafika milioni 100" amesema 

Mmoja wa walionusurika, Mohammed Rashid amesema moto huo umeteketeza kila kitu ikiwamo Sh300, 000 na nguo zake zote.

Kwa upande wake balozi wa eneo hilo, Kundandumi Kanuya amesema kuwa moto huo ulizuka alfajiri baada ya wapita njia kuona ukitokea katika chumba kimoja wapo na kuteketeza Kila kitu huku wageni waliokuwa wamelala wakiokolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano na ikibainika ni yeye hatua zaidi zitachukuliwa.

"Nikweli tukio hilo lipo na kikosi cha zima moto walifanikiwa kudhibiti moto huo usisambae eneo linguine na mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano na kithibitisha ni yeye aliyeusababisha atachukuliwa hatua "amesema

Chanzo: www.mwananchi.co.tz