Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sita mbaroni kwa kushindwa kuuza sukari kwa bei elekezi

Pingu Law Sita mbaroni kwa kushindwa kuuza sukari kwa bei elekezi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, linawashikilia wafanyabiashara sita wa sukari kwa tuhuma za kuuza sukari kinyume na bei elekezi ya serikali.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme, katika kikao alichofanya na wafanyabiashara wa sukari mkoani humo kilichokuwa na lengo la kujua changamoto zinazowakumba wafanyabiashara hao na kuwasababisha kushindwa kuuza bei elekezi ya serikali.

Mndeme amesema mkoani humo kuna tatizo la bei ya sukari kutokuwa rafiki wa walaji, hivyo ameona akutane na wafanyabiashara hao ili kuzungumza nao kujua tatizo nini hadi kushindwa kuuza sukari kwa bei elekezi ya serikali.

Amesema serikali imetoa maelekezo na kila Kanda imetolewa bei elekezi ambapo Kanda ya Ziwa ukiwamo Mkoa wa Shinyanga, kwamba bei ya jumla ni Sh. 2,600 hadi 2,800, rejareja Sh. 2,800 hadi 3,000 na kwamba mlaji wa sukari kwa mkoa huo wa Shinyanga anauziwa sukari kilo moja Sh. 3,200 hadi 5,000.

“Kunanini kwa wafanyabiashara mnashindwa kuuza sukari kwa bei elekezi ya serikali, mnaficha sukari na kwanini mpaka tunafikia hatua ya kukamatana, na mpaka sasa tumewakamata wafanyabiashara sita kutoka Kahama, watatu wakubwa, watatu wadogo kwa kwenda kinyume na maelekezo ya serikali ya kuuza sukari kwa bei elekezi,” amesema Mndeme.

“Hii kamatana kamatana, vutana vutana, nikaona hapana ngoja tukae tuzungumze tujue kwanini wafanyabiashara hawa wanauza sukari kinyume na bei elekezi, kwanini wanaficha sukari kwanini hawaendi kununua sukari, ndipo nikaona tukutane tuongee lasivyo tutawakamata wote,” ameongeza Mndeme.

Amesema serikali imetoa ushuru kwenye sukari impot duty asilimia 35, VAT asilimia 18 ili bei iwe rafiki, lakini bei haishuki ipo vile vile huku wilayani Kahama kukiwa hakuna sukari, tofauti na Kishapu na Shinyanga.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wamesema kwamba tatizo siyo wao ambao wanasababisha bei ya sukari kuwa juu, bali ni kwenye viwanda na maeneo ambayo wanauziwa sukari hiyo, kuwa bei elekezi ya serikali haiendani na uhalisia wa bei ya sokoni.

Wametolea mfano mfuko wa sukari Kilo 25 bei elekezi ya serikali inasema uuzwe kwa Sh. 70,000 lakini wao wanauziwa Sh.75,500, na kutoa ushauri kwa serikali kwamba wanapopanga bei elekezi washirikishe wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara, ushauri ambao mkuu wa mkoa ameahidi kuufanyia kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live