Iringa. Kati ya matunda ambayo huwezi kuyakosa katika mitaa mbalimbali ya mji wa Iringa ni matunda pori.
Baadhi ya matunda hayo ni songwe, mikusu, misasati, misaula, misada na matowo.
Wafanyabiashara wa matunda hayo wanasema kadri siku zinavyokwenda ndivyo idadi kubwa ya watu wanayachangamkia kwa imani kwamba ni kinga ya baadhi ya magonjwa.
Mmoja wa wafanyabiashara wa matunda hayo katika eneo la Uhindini, Daines Keneth amesema watu wengi wanayapenda wakiamini ni tiba ya magonjwa kwa kuwa mimea yake huchepua bila hata kupandwa au kuwekewa mbolea.
“Kwa siku nauza kati ya bakuli 20 au 30 za misasati. Bakuli moja nauza Sh1,000 na ni matunda ambayo naokota porini,” amesema.
Mpenzi wa matunda hayo, Ignas Ndezi amesema anayapenda kutokana na ladha yake, jinsi yanavyoweza kutibu magonjwa.
Pia Soma
- Vyama vya ushirika vyatumia fedha za wakulima kusafirisha pamba
- DC Temeke ataka siku moja zaidi tamasha la Jamafest
- VIDEO: Majaliwa amkalia kooni mkurugenzi manispaa Iringa ujenzi wa ukumbi eneo la shule
“Kuna faida nyingi za kula matunda licha ya kupenda ladha tamu za matunda tunayokula, matunda yana virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C.”
“Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo, kiharusi, shinikizo la damu, aina mbalimbali za saratani, matatizo ya macho na mengine mengi kwa hiyo nashauri watu wale matunda sio tu matunda pori,” amesema Dk Kilawa.