Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Sio wote wanaokufa Kilimanjaro sababu ni corona’ - Serikali Kilimanjaro

98f62a1b86ca7684c2d55bf038148d96.jpeg ‘Sio wote wanaokufa Kilimanjaro sababu ni corona’ - Serikali Kilimanjaro

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema siyo kweli kwamba kila anayefariki dunia katika mkoa huo ni kutokana na ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, bali yapo magonjwa mengine.

Aidha, imesema hakuna ukweli kwamba watu hao hufariki dunia katika ardhi ya mkoa huo, bali asilimia kubwa miili hurejeshwa mkoani hapa kutoka mikoa mingine walikofariki ikiwamo nje ya nchi.

Mkuu wa mkoa huo, Steven Kagaigai alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa uzinduzi wa chanjo ya corona katika mkoa huo ambao umetengewa chanjo dozi 60,000 na tayari watu 10,300 wameshachanja.

“Kuna taarifa potofu zinasambaa katika mitandao ya kijamii kuwa kila siku watu wanazikwa mkoani hapa kwa covid-19, siyo kweli kuwa wote wanakufa kwa ugonjwa huo na wamefia hapa Kilimanjaro,” alisema.

Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa alisema takwimu zinazoonesha mkoa wa Kilimanjaro una wagonjwa wengi, lakini hali hiyo pia inachangiwa na uwapo wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC.

“Lazima pia tutambue siyo kila anayeugua covid-19 hufariki dunia, lazima wataalamu wetu mtoe elimu katika jambo hilo ili kutoipotosha jamii na kuijengea hofu,” alisema.

Kagaigai alisema kutokana na mila na desturi za makabila ya mkoa huo, husafirisha miili ya wapendwa wao kokote kule duniani na kuzikwa katika mashamba yao mkoani hapa ndio maana huonekana kuwa na misiba mingi.

Alivitaka vyombo vya dola kukabiliana na wanaopotosha kwa makusudi kuhusu chanjo ya corona huo na ofisi yake ipo tayari kusaidia uandaaji wa mashtaka kwa watu hao.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kilimanjaro, Patrick Boisafi aliiomba jamii ya mkoa huo kubadili utamaduni wa kuleta miili ya wapendwa wao mkoani hapa na badala yake kuzika maeneo walikoishi kabla ya kifo kipindi hiki cha janga la

corona.

“Sina lengo la kupinga utamaduni huo, bali kulingana na ukuaji wa maendeleo ipo haja ya jamii kulitizama jambo hilo kwa mapana

Chanzo: www.habarileo.co.tz