Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sintofahamu mwewe anayekwapua fedha, vyakula Mtwara

Mwewe Ajabu.png Sintofahamu mwewe anayekwapua fedha, vyakula Mtwara

Sun, 5 Nov 2023 Chanzo: Mwananchi

Mtwara. Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nalingu Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wamepata hofu kwa zaidi ya mwezi sasa baada ya kutokea mwewe wa ajabu anaekwapua vyakula na fedha huku akiwakwarua kwa kucha baadhi ya watoto na watu wazima wakati akiwanyang’anya vitu hivyo.

Akizungumza kijijini hapo Issa Said Mkazi wa Nalingu anasema kuwa licha ya kuweka mitego ya vyakula vyenye sumu yakiwemo maandazi lakini mwewe huyo wameshindwa kumtega.

Anasema kuwa mwewe huyo ni wa ajabu mara kadhaa amekuwa akionekana maeneo ya sokoni na kunyang’anya watu vyakula na sasa amegeukia kwenye pesa.

“Yaani mwewe huyu hategeki na hapatikani kwa urahisi nimejaribu kumnasa lakini nilishindwa watoto wanahangaika sana mpaka kuna siku moja niliweka andazi sumu nikampa mtoto akashika lakini wala hakumkwapua”

“Mimi nina uhakika hawezi kuwa mwewe wa kawaida hatujawahi kusikia juu ya mwewe wa aina hii anachukua hadi pesa anapeleka wapi yaani mwewe anatishia amani hatuwezi kuwatuma watoto sokoni yaani wamekuwa ‘wakipaluliwa’ (kwaruzwa) mikono na wanavidonda,” anasema Said

Naye Bahati Hamis Kmkazi wa Kijiji cha Milamba, Kata ya Nalingu anasema mtoto wake amenyang’anywa mara kadhaa fedha na vitu vingine na m,wewe huyo.

“Huyu mwewe leo kamnyang’anya mtoto wangu sambusa yaani amekuwa anatufanya tuishi kwa shida siku ya kwanza alimkuta mtoto nyumbani na siku ya pili pia akamuachia na vidonda baada ya kumparua na kucha” anasema Hamis

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Nalingu, Mohamed Naivalula anasema kuwa wananchi wengi wamelalamika na mimi nimeshuhudia ni kweli mwewe huyo yupo na amesababisha wazazi kuwa hofu ya kutuma watoto dukani.

“Hili jambo ni kweli mwewe yupo anakwapua maandazi, chapati na pesa anachukua na pesa haikurudi tena na maandazi anayohukua hatujui anapeleka wapi hata ukingangania kitu anakupalua na kucha inakuwa ajue pesa yeye akishika anangangania kuna mama mmoja alimchukulia sh5000 na haikurudi hatuelewei ni mwewe kweli? fedha swali kubwa ni kwamba anapeleka wapi anawapa hofu wananchi” anasema Naivalula

Chanzo: Mwananchi