Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida kutumia maji ya Ziwa Victoria

Maafisa Wa Polisi Watoweka Baada Ya Boti Kuzama Katika Ziwa Victoria Singida kutumia maji ya Ziwa Victoria

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo October 17, 2023 amezindua rasmi Mradi Mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria hadi eneo la Shelui Mkoani Singida ambao umegharimu Tsh. bilioni 24.47 ikiwa ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Exim nchini India.

Mradi huu kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji ulikamilika tangu August 11, 2023 kwa gharama ya Tsh. bilioni 24.47 na Wananchi elfu arobaimi wa Vijiji vya Tinde-Shinyanga na Shelui-Singida tayari wanapata huduma ya maji safi na salama, ambapo utekelezaji wa awamu ya pili utagharimu Tsh. bilioni 16.2.

Ujenzi wa mradi huu unasimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Kahama (KASHWASA) ambapo hafla ya Uzinduzi wa Mradi huu Mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwemo, Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, Balozi wa India nchini Tanzania, Binaya Srikanta Pradhan, Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live