Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simulizi baadhi ya wanaume kukimbia tohara

Tohara Kwa Wanaume?fit=560%2C330&ssl=1 Simulizi baadhi ya wanaume kukimbia tohara

Thu, 16 May 2024 Chanzo: Mwananchi

Baadhi ya wanaume Manispaa Bukoba mkoani Kagera wameitaka Serikali kutafuta njia mbadala ya kuwafanyia tohara bila kupata maumivu.

Wanaume hao wametoa kauli hiyo, baada ya kutojitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya kufanyiwa tohara.

Tumaini Simon, mkazi wa Kata ya Bilele, Manispaa ya Bukoba akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumatano Mei 15,2024 amesema chanzo kinachosababisha wanaume walio wengi kushindwa kujitokeza vituo vya afya, zahanati na hospitali kwa ajili ya kufanyiwa tohara ni kuogopa maumivu baada ya kutahiriwa.

Kwa upande wake Rashidi Kambuga alikuwa na maoni tofauti ambapo amesema kuwa mwanaume anayeogopa kufanyiwa tohara kwa sababu ya maumivu atakuwa amekata tamaa ya maisha.

Takwimu tulizopata kutoka Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Bukoba zimeonyesha wanaume 1,088 wamepatiwa huduma ya tohara kinga mwaka 2023, huku lengo lilikuwa ni kuwafikia wanaume 2,820. Mwaka huu wana mpango wa kuwafikia wanaume 1,200 Manispaa ya Bukoba.

Muuguzi katika Hospitali ya Rufaa wilaya ya Bukoba kitengo cha Tohara Kinga, Eveline Rugabandala amesema kati ya wanaume wanaokutana nao wakati wa kutoa elimu juu ya tohara, wanaume 10 sita kati yao hawakubaliani na suala la kufanyiwa tohara.

Chanzo: Mwananchi