Matumizi mabaya ya simu ofisini, yametajwa kuwa chanzo cha rushwa za ngono kwa watumishi huku ikihusianishwa moja kwa moja na mmomonyoko wa maadili hasa kwa amabo hawatumii taaluma zao ipasavyo.
kauli hii imetolewa na mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa wataalamu wa utawala wa umma Tanzania(ATAP)
Shekimweri alitaja kundi linaloathirika zaidi na vitendo hivyo maofisini kuwa ni wasichana wanaokwenda kufanya elimu kwa vitendo.
Alisema kuna baadhi ya watawala wanajisifu kutembea na nusu ya watumishi wao ofisini jambo linalowafanya waonekane hawana sehemu za siri bali wanakuwa na sehemu za wazi kwa watumishi wao.
“Maadili yameporomoka katika baadhi ya watumishi wa umma. Kuna shida inayofanya wengine waishie kunung’unika wanapoona wenzao wanapanda kila uchwao japo walianza pamoja, lakini hawajiulizi sababu yake nini?”
Alihitimisha kwa kuwasihi watumishi wote wa umma kuzingatia maadili na utu kwani vyeo ni dhamana hivyo watumie uwakilishi wao vyema kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.