Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simiyu: Wenye vitambulisho vya Nida waongezeka

NIDA JULAI Simiyu: Wenye vitambulisho vya Nida waongezeka

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ZAIDI ya asilimia 80 ya wananchi sawa na wakazi 458,678 wa Mkoa wa Simiyu walio orodheshwa katika zoezi la usajiri wa vitambulisho vya taifa mkoani humo wamepata vitambulisho vyao, kwa mujibu wa Mamlaka Ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) mkoani Simiyu.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda amesema vitambulisho hivyo vitapelekwa katika ofisi za kata mbalimbali kulingana na mgawanyiko wa halmashauri husika hivyo kwa wale ambao hawajapata vitambulisho vyao wanatakiwa kutembelea ofisi za kata kwa ajili ya kupata vitambulisho.

“Leo tumeendelea na zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wananchi ambapo Asilimia 80 ya Wananchi wa wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wamepatiwa Vitambulsho vyao, hivyo kwa ambao bado hawajasajiliwa watumie fursa hii kujiandikisha ili kuvipata vitambulisho hivyo,” Dk Nawanda amewagiza watendaji wa vijiji.

Amesema kuwa wananchi waliopatiwa vitambulisho hivyo ni 458,678 ambapo kati yao 176,666 kutoka Wilaya ya Bariadi huku Wilaya ya Busega ikiwa na Wananchi 86,238 waliopata Vitambulisho hivyo ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ni 95,670 na 100,104 kwa Meatu.

Kwa upande wake, Afisa Usajili wa NIDA Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, Gloria Mwamafupa amesema kuwa vitambulisho hivyo vitasambazwa katika kata zote za halmashauri hiyo na baada ya mwezi mmoja wananchi hao wataweza kuviapata katika kata zao. - Naye Kamishna Msaidizi wa uhamiaji Mkoa wa Simiyu, Bazil Likasi amewasisitizia wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kwani kuwa na kitambulisho cha Taifa siyo suala la hiyari ni wajibu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kuwa nacho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live