Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simiyu: Kila ‘A’ Moja Tsh 50,000

Kafulila (2).jpeg RC Kafulila

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ametangaza nyongeza ya zawadi kwa mwalimu ambaye atafaulisha mwanafunzi kupata Daraja ‘A’ katika kila somo kwa shule za Sekondari mitihani ya kitaifa atapata zawadi ya Sh. 50,000 kwa 'A' moja.

Nyongeza ya zawadi hiyo itaanza kutumika kwenye matokeo ya mtihani wa kitaifa kidato cha nne mwaka huu, lengo likiwa kuongeza motisha kwa walimu pamoja na kuongeza ufaulu katika mkoa huo.

Kafulila amesema hayo leo, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na sita 2021 ambapo ameeleza malengo ya mkoa ni kupata A 2000.

Amesema kuwa awali zawadi kwa Mwalimu mweye A moja ilikuwa Sh. 10,000 ikapandishwa na kufikia 30,000, ambapo katika matokeo ya mwaka huu zawadi kwa ufaulu huo itakuwa Sh. 50,000.

" Nilipokuja Simiyu mwaka 2021 nilikuta mwalimu anapewa 10,000 kwa kila A ya mwanafunzi.

Nikahidi kuongeza kufikia 30,000 kwa kila A na walimu mkaongeza juhudi kiasi mkoa umeshika nafasi ya 3 kitaifa matokeo kidato cha 4 na zaidi idadi ya A za masomo imeongezeka kutoka 561 mpaka 958.

Huu ni ushahidj kwamba tukiongeza motisha tunaweza kupata A hata 2000 matokeo ya mwakani.. Hivyo naahidi kuongeza zawadi kwa kila A kutoka 30,000 mpaka 50,000.

“Kila Mwalimu atapewa kiasi hicho kama zawadi kulingana na A atakazopata, ukipata 50 utalipwa kila A moja Sh. 50,000 mara 50, ukipata 100 tutazidisha mara Sh 50,000,” Amesema Kafulila.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa licha ya Mkoa kushika nafasi ya tatu kitaifa matokeo ya kidato cha nne 2021, jumla ‘A’ zilipopatikana kwa masomo yote ni 958 kutoka 561 matokeo yaliyopita mwaka 2020.

Ameeleza kupata kwa kiwango hicho cha ufaulu, imetokana na kutangazwa kwa nyongeza ya zawadi kutoka Sh. 10,000 hadi 30,000, ambao ameemeza maelengo katika matokeo ya mwaka huu ni kupata ‘A’ 2000 kwa masomo yote.

Kafulila amewapongeza walimu na shule ambazo zilifanya vizuri kwenye matokeo hayo, licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo madeni ya walimu, ukosefu wa nyumba za kuishi, na miundombinu isiyokuwa rafiki.

“Licha ya changamoto hizo, hamkuweza kuvunjika moyo serikali itaendelea kutatua changamoto hizo lakini zisiwe kikwazo cha kushindwa kufikia malengo yetu ndani ya mkoa, tuendelee kufanya vizuri,” alisema Kafulila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live