Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wavamia vijiji, waua ng’ombe wanne

Simba Kijiji Simba Kijiji Simba wavamia vijiji, waua ng’ombe wanne

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hofu imetanga kwa wakazi wa Kijiji cha Magunga na Ihami Kata ya Mabogawilayani Iringa, baada ya kundi la simba kuvamia vijijini hivyo kwa nyakati tofauti na kuuwa ng'ombe wanne na kuwaacha wananchi wakiishi kwa uwoga kutokana na kuamini kuwa wanyama hao wanaweza kufanya shambulio lenye kuhusisha uhai wa binadamu.

Inadaiwa kuwa simba hao waliianza kuvamia kijiji cha Magunga, kisha kwenda Kijiji jirani cha Ihami na kuua ng’ombe hao wanne, hata hivyo tayari wanakijiji pamoja na askari wa wanyamapori wameungana kuwasaka wanyama hao.

Akizungumzia tukio hilo, Mfugaji Felix Malekela anasema baada ya kusikia vurugu ndani ya zizi alifuatilia na kukuta kundi kubwa la simba ndipo alipoanza kipiga kelele akisaidiana na majirani hali iliyowafanya wakimbie japo Tayari ngombe wameshaliwa.

"kinyesi cha ng'ombe tu ndicho kilichobakia mpaka sasa, simba hao wamekula kila kitu" amesema Malekela.

Nae bibi Mgovano ambaye ng'ombe zake zimeliwa na simba hao amesema alisikia mbwa zinabweka huku zinakimbia hivyo alihisi kuna shida lakini kutokana na umri wake wa uzee alishindwa kufanya lolote.

Bibi Mgovano amesema kulivokucha asubuhi hakukuta ng'ombe na baada ya kupiga kelele majirani walipofika ndipo kufanya utafiti na kugundua kuna miguu ya simba ndiyo iliyopita.

Bibi huyo anayeishi peke bila mtoto wala mume wake amesema anaamini simba hao ni wanyama tu na anaiomba serikali wamfikirie siku hizi mbili tatu kwani ng'ombe hao ndio walikuwa tegemeo la kila kitu kwake.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Maboga Venserus Muyinga amesema tukio hilo ni la pili lilitokea, mwaka 1981 katika kata kuliwahi kutokea tukio la ng’ombe kuliwa na wanyama mwitu hata hivyo hili la kuvamiwa na simba halikuwahi kutokea.

Muyinga amesema katika tukio hilo lilivotokea alichukua hatua ya kupiga simu kwa watu wanaohusika na wanyama na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa na kupatiwa msaada wa vikosi viwili askali wa maliasili ambavyo bado vinafanya kazi kuwasaka simba hao.

Muyinga ameendelea kuwaomba wanakijiji wenzake kuwa macho na wageni hao hatari kwani wanahatarisha maisha ya binadamu na mifugo pia.

"Jamani tutulie huyu mgeni wetu ni mkali hakuna asiyefahamu, na leo wanaweza kuwa kijiji hiki kesho kijiji kingine," alisema Muyinga

Nae balozi wa kijiji hicho cha Ihami Speransia Dalu amewaomba wananchi kutotembea hovyo hovyo kutokana na hali inayoendelea katika kata hiyo.

Kwa upande wao wananchi wameomba kupewa msaada zaidi ili simba hao wasiweze kuendelea na uharibifu katika kijiji chao.

Pia wameshukuru uongozi wa Serikali na Diwani wa Kata hiyo kwa kuweza kufanikisha zoezi la watu wa maliasili kufika mapema ili kuwasaka simba hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live