Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wavamia makazi ya watu Njombe

Eeeee Ngombee Simba wavamia makazi ya watu Njombe

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa kijiji cha Kijombe wilayani Wangingombe mkoani Njombe wamejikuta kwenye taharuki baada ya Simba wawili kuvamia makazi yao usiku wa kuamkia juzi Julai 22/2023 na kuua ng'ombe watano kijijini hapo.

Kufuatia tukio hilo kamati ya ulinzi na usalama imelazimika kufika kijijini hapo ikiongozwa na Claudia Kitta ambaye ni mkuu wa wilaya na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ambapo anakiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa rai kwa wananchi kutotembea usiku kipindi ambacho wanyama hao wakali wanatafutwa.

Kwa upande wake ofisa wanyama pori hifadhi ya Mpanga Kipengere Diminick Rwebangira ametoa pole kwa waliyoathiriwa na uvamizi wa wanyama hao na kuwataka kuchukua tahadhali

Chanzo: www.tanzaniaweb.live