Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wavamia kijiji, waua ng’ombe 16

82888 Pic+simba Simba wavamia kijiji, waua ng’ombe 16

Tue, 5 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti.  Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori, halmashauri ya wilaya ya Serengeti na wakazi wa kijiji cha Robanda wanaendesha msako wa ng'ombe ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa baada ya kutawanyika kufuatia kundi la simba kuvamia mazizi ya ng'ombe.

Katika tukio hilo ng'ombe 16 mpaka sasa wamethibitika kuuawa na watatu kujeruhiwa huku kundi kubwa la mifugo likiwa halijulikani lililopo.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu leo Jumatatu Novemba 4, amesema ameagiza askari wa Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) kutoka Ikorongo na afisa wanyamapori wilaya. "Nimewaambia baada ya msako wanipe taarifa kamili ya waliouawa, kujeruhiwa, kupotea na waliopatikana," amesema.

Ofisa wanyamapori wilaya John Lendoyani amesema hadi sasa wako porini wanaendelea na msako,"kwa ujumla wametawanyika na kukimbilia maeneo tofauti tofauti, wapo baadhi wanarudi wenyewe, nitakuwa na idadi kamili baada ya zoezi zima,"amesema.

Akizungumzia tukio hilo, mfugaji Samweli Mahewa anasema baada ya kusikia vurugu ndani ya zizi alifuatilia na kukuta kundi kubwa la simba ndipo alipoanza kipiga kelele akisaidiana na majirani hali iliyowafanya simba hao kukimbia.

“Mizoga mpaka sasa imefikia 16 inawezekana bado ipo mingine tunaendelea kutafuta,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz